Nasa kwa haraka unachowaza na ukumbushwe baadaye ukiwa katika eneo au wakati unaofaa. Tamka memo ya sauti popote ulipo na itanukuliwa kiotomaki. Piga picha ya bango, stakabadhi ya malipo au hati na uipange kwa urahisi au uipate baadaye katika utafutaji. Google Keep hurahisisha hatua ya kunakili unachowaza au orodha yako na kuishiriki na marafiki na familia.
Nakili unachowaza
• Weka madokezo, orodha na picha kwenye Google Keep. Je, huna muda? Rekodi memo ya sauti na Google Keep itainukuu ili uweze kuipata baadaye.
• Changamkia wijeti kwenye kompyuta kibao na simu yako na uweke vigae na madoido kwenye kifaa chako cha Wear OS ili unase unachowaza haraka.
Shiriki mawazo na marafiki na familia
• Panga kwa urahisi sherehe ya ghafla kwa kushiriki madokezo yako ya Google Keep na wengine na kushirikiana nao katika muda halisi.
Pata unachohitaji, haraka
• Paka rangi na uweke lebo kwenye madokezo ili uyapange kwa haraka na ufanye mambo yako mengine. Ikiwa unahitaji kupata kitu ulichohifadhi, utakipata kwa kutafuta kwa urahisi.
• Bandika madokezo kwenye skrini ya kwanza ya kompyuta kibao au simu yako ukitumia wijeti na uweke njia za mkato kwenye madokezo yako ukitumia vigae katika kifaa cha Wear OS.
Unaweza kuifikia kila wakati
• Google Keep hufanya kazi kwenye simu, kompyuta kibao, kompyuta na kifaa chako cha Wear OS. Kila kitu unachoongeza husawazishwa kwenye vifaa vyako vyote kwa hivyo utapata unachowaza kila wakati.
Dokezo sahihi kwa wakati unaofaa
• Unahitaji kukumbuka kununua bidhaa za dukani? Weka kikumbusho kinachotegemea mahali ili uonyeshwe orodha yako ya bidhaa unazohitaji ukifika dukani.
Inapatikana kila mahali
• Jaribu Google Keep kwenye wavuti katika http://keep.google.com na uipate katika Duka la Chrome kwenye Wavuti kupitia http://g.co/keepinchrome.
Ilisasishwa tarehe
9 Jan 2025