Gboard ina kila kitu unachopenda kuhusu Kibodi ya Google—kasi na kutegemeka, Kuandika kwa Kutelezesha Kidole, kuandika kwa kutamka, Kuandika kwa mkono na zaidi
Kuandika kwa Kutelezesha Kidole — Andika kwa haraka kwa kutelezesha kidole chako kutoka herufi moja hadi nyingine
Kuandika kwa kutamka — Tamka maandishi kwa urahisi popote ulipo
Kuandika kwa mkono* — Andika kwa herufi zilizoviringwa na zilizochapishwa
Kutafuta Emoji* — Pata emoji unayoitaka kwa haraka
GIF* — Tafuta na ushiriki GIF ili utoe maoni bora zaidi.
Kuandika katika lugha nyingi — Huhitaji kubadili lugha mwenyewe. Gboard itapendekeza na kusahihisha kiotomatiki kutoka lugha zozote zinazotumika.
Google Tafsiri — Tafsiri unapoandika kwenye kibodi
* Haitumiki kwenye vifaa vya Android Go
Mamia ya aina za lugha, ikiwa ni pamoja na:
Kiafrikana, Kiamhariki, Kiarabu, Kiasami, Kiazabajani, Kibavaria, Kibengali, Kibhojpuri, Kibumizi, Kisebuano, Kichatisgarhi, Kichina (Kimandarini, Kikantoni na nyinginezo), Kichitagonia, Kicheki, Kidekani, Kiholanzi, Kiingereza, Kifilipino, Kifaransa, Kijerumani, Kigiriki, Kigujarati, Kihausa, Kihindi, Kiigbo, Kiindonesia, Kiitaliano, Kijapani, Kijava, Kikannada, Kikhema, Kikorea, Kikurdi, Kimagahi, Kimaithili, Kimalesia, Kimalayalam, Kimarathi, Kinepali, Kisotho cha Kaskazini, Kiodia, Kipashto, Kiajemi, Kipolandi, Kireno, Kipunjabi, Kiromania, Kirusi, Kisaraiki, Kisindhi, Kisinhala, Kisomali, Kisotho cha Kusini, Kihispania, Kisunda, Kiswahili, Kitamili, Kitelugu, Kitai, Kitswana, Kituruki, Kiukraini, Kiurdu, Kiuzibeki, Kivietinamu, Kikhosa, Kiyoruba, Kizulu na nyingine nyingi! Tembelea https://goo.gl/fMQ85U ili upate orodha kamili ya lugha zinazotumika
Vidokezo muhimu:
• Kidhibiti cha kishale cha ishara: Telezesha kidole chako kwenye upau wa nafasi ili usogeze kishale
• Kufuta ishara: Telezesha kushoto kutoka kitufe cha kufuta ili ufute kwa haraka maneno mengi
• Fanya safu ya nambari ipatikane kila wakati (washa katika Mipangilio → Mapendeleo→ Safu ya Nambari)
• Vidokezo vya alama: Onyesha vidokezo vya haraka kwenye vitufe vyako ili ufikie alama kwa kubonyeza kwa muda mrefu (washa katika Mipangilio → Mapendeleo → Bonyeza kwa muda mrefu ili upate alama)
• Hali ya kutumia kwa mkono mmoja: Kwenye simu zenye skrini kubwa, bandika kibodi upande wa kushoto au kulia kwenye skrini
• Mandhari: Chagua mandhari yako mwenyewe, yenye mipaka au yasiyo na mipaka muhimu
Ilisasishwa tarehe
8 Jan 2025