Google Messages ndiyo programu rasmi ya Google ya kutuma ujumbe. Google Messages inabadilisha jinsi watumiaji bilioni moja wanavyowasiliana na inaendeshwa na Huduma za Mawasiliano Maalum (RCS), kiwango cha sekta cha kutuma ujumbe kinachochukua nafasi ya SMS na MMS. Ukitumia RCS, unaweza kutuma picha na video zenye ubora wa juu, kufurahia magumzo nyumbufu ya kikundi na kuwasiliana na watumiaji wengine wa RCS kwa urahisi ikijumuisha marafiki zako wanaotumia iPhone.
• Huduma ya Mawasiliano Maalum: Tuma picha na video zenye ubora wa juu, ona marafiki zako wanapoandika, na ufurahie magumzo nyumbufu ya kikundi ambayo sasa yanajumuisha kwa urahisi marafiki zako wanaotumia iPhone.
• Kuweka Upendavyo: Weka mazungumzo yako upendavyo ukitumia vipengele kama vile rangi maalum za viputo vya gumzo au GIF za selfi.
• Masuala ya Faragha: Usiwe na wasiwasi ukifahamu kuwa mazungumzo yako binafsi yanalindwa kwa usimbaji fiche wa mwanzo hadi mwisho kati ya watumiaji wa Google Messages, kwa hivyo hakuna yeyote (ikijumuisha Google na washirika wengine) anayeweza kusoma au kuona ujumbe na viambatisho vyako isipokuwa mtu unayetumia ujumbe. Pia, furahia mipangilio ya ulinzi wa hali ya juu dhidi ya taka.
• Kipengele cha Kutuma Ujumbe Kinachotumia AI: Andika ujumbe mahiri ukitumia vipengele vyetu vipya zaidi vya AI na mapendekezo ya Uandikaji Mahiri.
• Urahisi wa Kupiga Gumzo Kwenye Vifaa: Anzisha gumzo kwenye simu yako na uliendeleze kwa urahisi kwenye kompyuta au kishikwambi chako. Programu pia inapatikana kwenye Wear OS.
Kando na kutuma ujumbe, Google Messages ni njia bora zaidi, salama na dhahiri zaidi ya kuwasiliana.
Programu pia inapatikana kwenye Wear OS. Upatikanaji wa RCS hutofautiana kulingana na eneo na mtoa huduma na huenda ukahitaji kifurushi cha data. Upatikanaji wa vipengele hutofautiana kulingana na soko na kifaa na huenda ukahitaji kujisajili kwenye jaribio la beta.
Ilisasishwa tarehe
17 Des 2024