Programu ya Gemini ni kiratibu kinachotumia AI.
Programu ya Gemini inapatikana tu kwenye simu za Android zenye RAM ya GB 2 au zaidi, zinazotumia toleo la Android 10 na matoleo mapya zaidi.
Programu hii rasmi ni ya bila malipo. Gemini hukuwezesha utumie mifumo bora zaidi ya Akiliunde kutoka Google moja kwa moja katika simu yako ili uweze:
- Kupata usaidizi wa kuandika, kujadili ili kuzalisha mawazo, kujifunza na zaidi
- Kuandaa muhtasari na kupata maelezo ya haraka kutoka kwenye Gmail au Hifadhi ya Google
- Kuzalisha picha kwa haraka
- Kutumia maandishi, sauti, picha na kamera yako kupata usaidizi kwa njia mpya
- Kupanga safari ukitumia Ramani za Google na Ndege kwenye Google
Ikiwa unaweza kutumia Gemini Advanced itapatikana hapa kwenye programu ya Gemini.
Programu ya Gemini ya vifaa vya mkononi inasambazwa kwenye maeneo, lugha na vifaa mahususi. Pata maelezo zaidi kuhusu upatikanaji kwenye Kituo cha Usaidizi:
https://support.google.com/?p=gemini_app_requirements_android
Soma Ilani ya Faragha ya Programu za Gemini:
https://support.google.com/gemini?p=privacy_notice
Ilisasishwa tarehe
19 Nov 2024