Habari mpya katika kesi hii inamfanya Roland kuangalia tena mauaji ya mlinzi yule wa jela. Kwa sasa ana uhakika kuwa anamfahamu Uwe Finch na anaamua kumfahamisha Anne Larsen. Anne ndiye alipata michoro ya vidole vya Uwe Finch, na kwa muda uliopita, Roland ametambua kuwa Anne anaweza kuwa mtu wa msaada mkubwa katika uchunguzi wa polisi. Bertram anashtuka kutambua kilichomfanyikia mama yake ila kwa mara moja Anne Larsen, mwanahabari kutoka TV2 East Jutland, anafika. Bertram anaangua kilio mbele ya Anne huku akimueleza mambo yote na Anne anamuambia kuwa wanahitaji kuondoka mara moja. Ila muda umeyoyoma. Wakati Roland anasikia kuhusu kifo kipya kupitia redio ya gari lake anahofia kuwa huenda Anne Larsen ako hatarini pia na anajaribu kumpigia simu ila hapati majibu. Anapopokea simu, anatumai kuwa ni Anne ila inageuka na kuwa ni Leif Skovby, ofisa mmoja katika kesi ile ya mauaji. Leif anataka kuonana naye Roland, na kile anachomwambia kinafanya mambo yote kubainika. Roland anamtumia ofisa huyu kumsaidia kupata simu ya Anne ila, je, Roland atampata Anne kabla ya muda kuyoyoma?
The Cleaner ni mchezo wa kuigiza wa kihalifu wenye matukio sita.
Inger Gammelgaard Madsen (b. 1960) ni mwandishi kutoka nchi ya Denmark. Inger Gammelgaard Madsen ana uasilia wa kisomo cha uchoraji wa vielelezo. Alianza kuandika hadithi zinazohusu uhalifu "Dukkebarnet" katika mwaka wa 2008. Baada ya kitabu hiki, ameandika vitabu vingine kadhaa vinavyohusu uhalifu. Baadhi ya vitabu hivi ni "Drab efter begæring" (2009), "Slangers gift" (2014), "Dommer og bøddel" (2015) na "Blodregn" (2016).