WhatsApp Messenger

4.3
Maoni 202M
5B+
Vipakuliwa
Daraja la maudhui
PEGI 3
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini

Kuhusu programu hii

WhatsApp kutoka Meta ni programu ISIYOLIPISHWA ya kutuma ujumbe na kupiga simu za video. Inatumiwa na zaidi ya watu bilioni 2 katika zaidi ya nchi 180. Ni njia rahisi, ya hakika na faragha ya kutuma ujumbe, kwa hivyo unaweza kuwasiliana na ndugu na marafiki kwa wepesi. WhatsApp inafanyakazi kwenye vifaa vya mkononi na kompyuta hata kama muunganisho ni wa polepole, hutakiwi kulipa ada ya kujisajili*.

Njia ya faragha ya kutuma ujumbe kote duniani

Ujumbe na simu zako za binafsi kwenda kwa ndugu na marafiki hufumbwa mwisho hadi mwisho. Hakuna mtu nje ya mawasiliano yenu, hata WhatsApp yenyewe, anaweza kuyasoma au kuyasikiliza.

Miunganisho rahisi na salama, papo hapo

Unachohitaji ni nambari yako ya simu tu, huhitaji jina la mtumiaji au vitambulishi vya kuingia. Unaweza kuona watu unaowasiliana nao ambao tayari wanaitumia WhatsApp halafu uanze kuwatumia ujumbe.

Simu za sauti na video za ubora wa juu

Piga simu salama za sauti na video zinazowajumuisha hadi watu 8 bila malipo*. Unaweza kupiga simu kati ya vifaa vya mkononi kwa kutumia Intaneti ya simu yako, hata muunganisho ukiwa wa polepole.

Soga za vikundi ili uendelee kujumuika

Endelea kujumuika na ndugu na marafiki. Soga za vikundi zilizofumbwa mwisho hadi mwisho hukuwezesha kutuma ujumbe, picha, video na hati kati ya vifaa vya mkononi na kwenye kompyuta.

Ungana mubashara

Shiriki mahali ulipo na watu ulio nao katika soga ya binafsi au ya kikundi pekee, pia unaweza kuacha kushiriki wakati wowote. Au, rekodi ujumbe wa sauti kwa mawasiliano ya haraka.

Shiriki matukio ya kila siku katika sehemu ya Hali

Hali inakuruhusu kushiriki masasisho ya maandishi, picha, video na GIF zitakazotoweka baada ya saa 24. Unaweza kuchagua kushiriki hali yako na watu wote unaowasiliana nao au wachache tu unaowachagua.

Tumia WhatsApp kwenye saa yako ya Wear OS ili kuendelea na mazungumzo, kujibu ujumbe na kupokea simu - yote kwenye mkono wako. Na, ongeza vigae na matatizo ili kufikia gumzo zako na kutuma ujumbe wa sauti kwa urahisi.


*Unaweza kulipishwa kutumia data. Wasiliana na mtoa huduma wako kwa maelezo.

---------------------------------------------------------

Ikiwa una maswali au maoni, tafadhali nenda kwenye WhatsApp > Mipangilio > Usaidizi > Wasiliana nasi
Ilisasishwa tarehe
7 Jan 2025

Usalama wa data

Usalama huanza kwa kuelewa jinsi wasanidi programu wanavyokusanya na kushiriki data yako. Faragha ya data na mbinu za usalama zinaweza kutofautiana kulingana na matumizi yako, eneo ulilopo na umri wako. Msanidi programu ametoa maelezo haya na anaweza kuyasasisha kadiri muda unavyopita.
Hakuna data inayoshirikiwa na wengine
Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi wasanidi programu wanavyobainisha kushiriki data
Programu hii huenda ikakusanya aina hizi za data
Mahali, Taarifa binafsi na nyingine5
Data inasimbwa kwa njia fiche inapotumwa
Unaweza kuomba data hiyo ifutwe

Ukadiriaji na maoni

4.3
Maoni 198M
Edensundjuma Afidhi
6 Januari 2025
Whatsapp yangu inakua inajifunga mazima nifanyeje malafiki
Watu 5 walinufaika kutokana na maoni haya
Je, maoni haya yamekufaa?
Joyce
4 Januari 2025
Nafunguwa whatsapp inagoma ndo nin maelekezo mnatoa tunafata lakini hakuna kinachotendeka nimehangaika hadi nakata tamaa jamani
Watu 68 walinufaika kutokana na maoni haya
Je, maoni haya yamekufaa?
Meshack Samwel
8 Januari 2025
Kufungua akaunti ya whatsapp
Je, maoni haya yamekufaa?

Vipengele vipya



• Sasa, unaweza kuhariri ujumbe ndani ya dakika 15 baada ya kuutuma. Bonyeza ujumbe kwa muda kisha uchague "Hariri" ili uanze mchakato wa kuuhariri.
• Soga za vikundi huonyesha picha za jalada za washiriki walio kwenye soga.

Vipengele hivi vitazinduliwa katika wiki zijazo. Asante kwa kutumia WhatsApp!