Jipatie pesa kwa kukamilisha task rahisi kama vile: kutoa maoni yako, kukamilisha dodoso fupi au kupiga picha ndani ya mji wako. Soko la kazi la Premise linakua kila siku, kwahiyo kuna task kwaajili ya watu wote. Jiunge na maelfu ya wachangiaji wa Premise wanaojipatia kipato kila siku kwa kuchangia ufahamu wao kuhusiana na jamii yao.
Licha ya kuweza kupakua app ya Premise kila pahala, kwa sasa tasks hazipatikani katika kila mji. Tasks zinapatikana kutokana na mahitaji ya mashirika tunayofanya nayo kazi, kwa hiyo upatikanaji unaweza kubadilika mara kwa mara.
Kwanini uwe Mchangiaji wa Premise?
Nasa kinachotokea ndani ya jamii yako: Tumia simu yako ya Android kushiriki mawazo yako kuhusiana na uhalisia wa maisha yako, pamoja na jamii yako.
Jiingizie kipato sasa hivi: Lipwa kwa jitihada zako. Chagua tasks zinazoendana na muda uliyokuwa nao. Kadri unavyojituma zaidi ndivyo utakavyo jipatia kipato zaidi!
Mawazo yako yanaumuhimu: Wewe ni rasilimali yenye thamani, na mashirika pamoja na viongozi wa jamii wanathamini mawazo yako. Premise inarahisisha kunasa na kusambaza mawazo yako.
Shiriki taarifa za kweli zinazoweza kuleta mabadiliko ya kweli: Jiunge na mtandao unaokua, wenye maelfu ya wachangiaji katika kila kona ya dunia wanaokamilisha tasks kila siku zinazosaidia kutengeneza sera, bidhaa na huduma zilizobora zaidi kwa kila mtu.
Ahsante kwa kuwa Mchangiaji wa Premise!
Unahitaji msaada? Tutumie Barua pepe kwenda
[email protected]Jifunze zaidi kuhusiana na kuwa Mchangiaji wa Premise kupitia: www.premise.com/contributors