Plantix - daktari wa mazao

Ina matangazo
4.1
Maoni elfu 91.5
10M+
Vipakuliwa
Daraja la maudhui
PEGI 3
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini

Kuhusu programu hii

Ponya mazao yako na vuna mazao mengi zaidi kupitia Programu ya Plantix!

Plantix hubadilisha simu yako ya Android kuwa daktari wa mazao wa mkononi, unayeweza kumtumia kutambua kwa usahihi wadudu na magonjwa yaliyopo kwenye mazao ndani ya sekunde chache. Plantix huhudumu kama suluhisho kamili la uzalishaji na usimamizi wa mazao.

Programu ya Plantix hushughulikia mazao makuu 30 na hutambua uharibifu wa mimea zaidi ya 400 — kwa kupiga tu picha ya zao lenye ugonjwa. Hupatikana katika lugha 19 na imekwishapakuliwa zaidi ya mara milioni 10 . Hili huifanya Plantix kuwa programu #1 ya kilimo itumikayo kutambua uharibifu, kudhibiti wadudu na magonjwa pamoja na kuboresha mavuno kwa ajili ya wakulima duniani kote.

Plantix Inakupatia Nini

🌾 Ponya Mazao Yako:
Tambua wadudu na magonjwa yaliyopo kwenye mazao na pata matibabu yanayopendekezwa

⚠️ Taarifa za Magonjwa:
Kuwa wa kwanza kufahamu pale ugonjwa unapokaribia kuikumba wilaya yako

đź’¬ Jumuiya ya Wakulima:
Uliza maswali yanayohusiana na mazao na pata majibu kutoka kwa wataalamu zaidi ya 500 wa jumuiya

đź’ˇ Vidokezo vya Kilimo:
Fuata mbinu bora za kilimo kipindi chote cha msimu wa mazao yako

â›… Utabiri wa Hali ya Hewa ya Kilimo:
Tambua wakati mzuri wa kupalilia, kunyunyizia dawa na kuvuna

🧮 Kikokotoo cha Mbolea:
Kokotoa mahitaji ya mbolea ya mazao yako kulingana na ukubwa wa shamba

Tambua na Tibu Matatizo ya Mazao
Iwe mazao yako yanakabiliwa na wadudu, magonjwa au upungufu wa virutubisho, kwa kulipiga picha tu zao husika kwa kutumia programu ya Plantix, utapata uchunguzi wa zao hilo pamoja na matibabu yanayopendekezwa ndani ya sekunde chache.

Pata Majibu ya Maswali Yako Kutoka kwa Wataalamu
Wakati wowote ule unapokuwa na maswali yanayohusu kilimo, wasiliana na jumuiya ya Plantix! Nufaika na ujuzi wa wataalamu wa kilimo au wasaidie wakulima wenzako kupitia uzoefu wako. Jumuiya ya Plantix ni mtandao mkubwa zaidi wa kijamii wa wakulima na wataalamu wa kilimo duniani kote.

Ongeza Mavuno Yako
Vuna zaidi kutoka kwenye mazao yako kwa kufuata mbinu bora za kilimo na kutumia mikakati ya kinga. Programu ya Plantix hukupatia mpango wa utekelezaji wenye vidokezo vya kilimo kwa ajili ya msimu wote wa mazao yako.


Tembelea tovuti yetu katika
https://www.plantix.net

Jiunge nasi kwenye Facebook katika
https://www.facebook.com/plantix

Tufuate Instagram katika
https://www.instagram.com/plantixapp/
Ilisasishwa tarehe
18 Des 2024

Usalama wa data

Usalama huanza kwa kuelewa jinsi wasanidi programu wanavyokusanya na kushiriki data yako. Faragha ya data na mbinu za usalama zinaweza kutofautiana kulingana na matumizi yako, eneo ulilopo na umri wako. Msanidi programu ametoa maelezo haya na anaweza kuyasasisha kadiri muda unavyopita.
Programu hii huenda ikaruhusu aina hii ya data ikafikiwa na washirika wengine
Mahali, Shughuli za programu na Kifaa au vitambulisho vingine
Programu hii huenda ikakusanya aina hizi za data
Mahali, Taarifa binafsi na nyingine4
Data inasimbwa kwa njia fiche inapotumwa
Unaweza kuomba data hiyo ifutwe

Ukadiriaji na maoni

4.2
Maoni elfu 91