Opera Mini inahusu kasi na starehe, lakini ni zaidi ya kivinjari tu! Ni nyepesi na inaheshimu faragha huku ikikuruhusu kuvinjari intaneti haraka, hata kwenye mitandao ya kasi ya chini au iliyosongamana. Smart Browsing huteua hali bora ya uokoaji data kwa ajili yako uvinjari sana ukitumia mpango wako wa data.
Huzuia matangazo yanayoudhi na kujumuisha kidhibiti cha kupakua na kushiriki faili nje ya mtandao. Ni kichezaji maudhui rahisi cha hali inayokuwezesha kusikiliza muziki na kutazama video bila tatizo, huku kikikupa habari zinazokufaa zinazoendeshwa na AI.
Vipengele bora
• Okoa Data
Okoa 90% ya data yako na uvinjari haraka, hata mitandao ya kasi ya chini, bila kuchachawiza hali ya kuvinjari. Angalia hali ya uokoaji data kila siku kwa urahisi huku Opera Mini Smart Browsing ikiteua kiotomatiki kuvinjari kwa hali ya utumiaji wako bora.
• Upakuaji Mahiri
Kagua kiotomatiki tovuti za video na faili za muziki zinazopakulika na uzipakue chinichini. Pata vipakuliwa vyote na faili za awali kwa urahisi kwenye kifaa chako – hakuna kuchakura tena kwenye folda. Smart Downloading inajumuishwa na kichezaji video cha Opera Mini na Kushiriki Faili Nje ya Mtandao, uweze kupakua na kushiriki faili na marafiki!
• Kushiriki Faili Nje ya Mtandao
Tuma na upokee faili kwa njia salama bila mtandao wala matumizi data. Kipengele cha Kushiriki Faili Nje ya Mtandao kinaweza kuhamisha picha au faili kwa kasi hadi MB 300 na kulifanya kuwa suluhisho bora la kushiriki faili popote! Kagua msimbo wa QR na ushiriki na watumiaji wa Opera Mini haraka.
• Zuia Matangazo
Opera Mini ina kizuia matangazo cha ndani hivyo unaweza kuvinjari wavuti bila matangazo yanayoudhi na kukuza hali ya kuvinjari wavuti bila tatizo!
• Boresha Kivinjari Chako
WEWE ni Mkuu wa Opera Mini! Boresha kivinjari kikufae kwa kuchagua mpangilio, mandhari, kategoria za habari na zaidi. Ifanye Opera Mini yako ivutie!
• Habari Zinazofaa
Fuatilia habari zinazovuma za ndani na kimataifa haswa zinazokufaa. Mlisho wa habari uliozimwa na kuwashwa ndani ya Opera Mini unaendeshwa na mtambo wetu wa AI. Fuata idhaa unazopenda uone mada zinazokufaa.
• Kichezaji Video
Tazama na usikilize moja kwa moja, au pakua utumie baadaye. Kichezaji video cha Mini kina hali inayorahisisha matumizi kwenye kifaa chako cha mkononi kimejumuishwa na Download Manager.
• Kusoma Nje ya Mtandao
Hifadhi hadithi na kurasa za wavuti kwenye simu yako ukiwa kwenye Wi-Fi na uzisome baadaye nje ya mtandao bila data. Unaweza kuchagua kuonyesha upya kiotomatiki habari ukiwa na Wi-Fi na udhibiti kwa urahisi faili zilizohifadhiwa. Zifikie haraka kwa kuongeza njia mkato kwenye kipengele cha Kusoma Nje ya Mtandao katika upau wa kusogeza.
• Vinjari Faraghani
Opera Mini inakupa ulinzi mkubwa wa faragha kwenye wavuti. Tumia vichupo vyako vya faragha kuvinjari bila kuacha historia kwenye kifaa wala kufuatiliwa.
• Hali ya Usiku
Punguza mwangaza wa skrini ulinde macho unaposomea gizani.
Kujifunza zaidi kuhusu ruhusa ambazo Opera Mini hutumia, tembelea: http://www.opera.com/help/mini/android/permissions
Fanya zaidi na Opera: https://www.opera.com/mobile/android
Opera inaweza kuonyesha matangazo kutoka Facebook. Kujifunza zaidi, tazama: https://m.facebook.com/ads/ad_choices
Wasiliana:
Twitter – http://twitter.com/opera/
Facebook – http://www.facebook.com/opera/
Instagram – http://www.instagram.com/opera
Sheria na Masharti:
Kwa kupakua programu hii, unakubali Makubaliano ya Leseni ya Mtumiaji kwenye https://www.opera.com/eula/mobile. Unaweza kujifunza jinsi Opera inavyoshughulikia data katika taarifa ya Faragha kwenye https://www.opera.com/privacy.
Ilisasishwa tarehe
18 Des 2024