Microsoft To Do ni orodha rahisi na mahiri ya mambo ya kufanya ambayo hukuwezesha kupanga siku yako kwa urahisi. Uwe unapangia shughuli kazini, shuleni au nyumbani, To Do itakusaidia kutekeleza shughuli nyingi zaidi na kupunguza viwango vya mfadhaiko. Inajumuisha teknolojia mahiri na usanifu wa kupendeza ili kukupa uwezo wa kuunda utaratibu rahisi wa kazi kila siku.
Ratibisha na upange siku yako
Ratibisha shughuli zako za siku ukitumia Mapendekezo maizi ya To Do na ukamilishe majukumu muhimu zaidi, miadi au kazi unazohitaji kukamilisha, kila siku. To Do hulandanisha kati ya simu na kompyuta yako kwa hivyo unaweza kufikia ya kufanya ukiwa shuleni, ofisini au kwenye duka la mboga au hata ukiwa safarini popote ulimwenguni.
Shiriki orodha zako pamoja na familia na washirika wako
Kushiriki orodha huwawezesha mshirikiane kwenye orodha na majukumu sawa na kufikia malengo yenu kwa urahisi. Iwe unataka kushiriki orodha ya vipengee vyako vya kazi na timu zako au orodha ya manunuzi yako ya mboga na mpendwa wako, kwa kutumia kiungo chetu cha kushiriki, tunarahisisha kushirikiana kwenye timu ndogo na moja kwa moja. Kufanikisha shughuli kwa pamoja kumerahisishwa zaidi sasa!
Gawa majukumu yako yawe vipengee vidogo, vya kutekelezeka
Hatua (Majukumu madogo) hurusu to-do yoyote kugawika katika vipengee vidogo vinavyoweza kutekelezeka zaidi. Ili kuwasaidia wateja kuweza kutekeleza hata shughuli nyingi zaidi, kila to-do itaonyesha idadi kamili ya hatua (majukumu madogo) iliyo nayo na idadi ya hatua hizo ambazo tayari zimekamilishwa. Hatua (Majukumu madogo) zitasalia kwenye hali zao za kukamilika hata ikiwa to-do zinazotokana nazo itatiwa alama kuwa imekamilishwa au haijakamilishwa.
Weka tarehe za makataa na vikumbusho
Unaweza kuongeza haraka, kupanga na kuratibu mambo yako ya kufanya ukiwa popote pale. Ukiwa na mambo muhimu ya kufanya ambayo hakika hufai kusahau, unaweza kuongeza vikumbusho na tarehe za makataa – tutakusaidia kuyakumbuka. Ikiwa una mambo ya kufanya ambayo unahitaji kutia alama kila siku, wiki au mwaka, unaweza kuweka tarehe za kukamilisha zinazojirudia ili ujikumbushe kila wakati.
Ongeza madokezo kwenye majukumu yako
Unaweza pia kutumia To Do kama programu ya kuandika madokezo, kuongeza madokezo ya kina kwa kila mambo ya kufanya—kuanzia anwani mbalimbali hadi maelezo ya kina kuhusu kile kitabu unachotaka kusoma, hadi tovuti ya mkahawa unaopenda. Unaweza kukusanya majukumu yako yote pamoja na vidokezo mahali pamoja ili kukusaidia kufanikisha mengi.
Kuwekea orodha zako msimbo wa rangi
Je, ni masuala yapi maishani mwako ambayo ungependa kufanikisha zaidi? Unaweza kuwekea kila mojawapo ya orodha hizo msimbo wa rangi. Sasa unaweza kuongeza kazi zako za ziada kwenye orodha moja kwa haraka, kuongeza orodha yako ya mboga kwenye orodha nyingine, orodha yako ya ununuzi, miradi yako ya DIY ya nyumbani kwenye orodha zaidi sasa. Ikiwa unafuata mtindo kama ule wa GTD (Mbinu ya David Allen ya Kutekeleza Shughuli) basi unaweza kuandaa orodha ya Wakati fulani baadaye au orodha ya Kufuatilia shughuli.
Panga unachotaka kulenga kila asubuhi na ujihamasishe kwa uzalishaji thabiti kwa siku. Programu hii rahisi ya mambo ya kufanya orodha ya shughuli inapakuliwa na kutumiwa bila malipo. Inajumuisha mandhari yanayoweza kugeuzwa kukufaa, madokezo, vikumbusho, makataa, Mapendekezo maizi, na ulandanishaji katika vifaa vingi. Kwa ufupi, kila unachohitaji kudhibiti maisha yako na kufanikisha zaidi. Haijakuwa rahisi kukamilisha kazi zako au kazi zako za nyumbani. Ni zana ya usimamizi wa kazi unayohitaji kuongeza kwenye ghala la kila siku.
Kwa kusakinisha Microsoft To Do, unakubali masharti haya ya matumizi: https://go.microsoft.com/fwlink/?linkid=842577
Ilisasishwa tarehe
20 Jan 2025