MAENEO MENGI TOFAUTI
Jiunge na Akili kwenye matembezi ya usiku na mchana yenye kusisimua, akitembelea sehemu tofauti tofauti na kugundua kwamba ulimwengu una vitu vingi vya kuvutia!
Akili ataenda mahali gani kwengine? Msituni? Baharini? Atarudi nyumbani? Kwa kutumia kitabu hiki, uamuzi ni WAKO. Na usisahau kuwa fanya ndege wachezeshe mabawa yao,nyani wacheze na maboti yashindane!
Kutoka kwenye mawingu angavu mpaka kwenye bahari yakupendeza, tembelea ulimwengu wenye hadithi yenye kujenga.
VIPENGELE MUHIMU
* SOMA kupitia hatua tatu tofauti
* CHUNGUZA maneno, picha na mawazo kupitia vipengele tofauti tofauti
* SIKILIZA hadithi nzima na pia neno mojamoja
* CHAGUA Akili aaende wapi-- fanya hadithi iwe yako
* AKILI ndiye anaye hadithia hadithi yote
* FURAHIA kujifunza kusoma
KUPAKUA NI BURE, HAKUNA MATANGAZO WALA HUHITAJI KULIPA CHOCHOTE BAADA YA KUPAKUA APP
Kila kitu ni bure, imetengenezwa na Curious Learning na Ubongo, mashiriki yasiyo ya kiserikali.
KIPINDI CHA TELEVISION - AKILI AND ME
Akili and Me ni katuni zenye kuburudisha na kuelimisha kutoka Ubongo, watengenezaji wa Ubongo Kids na Akili and Me - vipindi vizuri vya kujifunza vilivyotengezwa Afrika kwa ajili ya Waafrika.
Akili ni mtoto mwenye miaka minne na mwenye udadisi, anaishi na famiia yake karibu na mlima Kilimanjaro, nchini Tanzania. Ana siri moja,kila usiku anapokuwa amelala, anaingia kwenye ulimwengu wa maajabu unaoitwa Lala land, ambako yeye na marafiki zake ambawo ni wanyama tofauti tofauti wanajifunza lugha, herufi, nambari na sanaa na wakati huohuo akijifunza ukarimu na kuanza kupatwa na hisia na mabadiliko ya haraka ya maisha ya mtoto mdogo! Vipindi vinarushwa katika nchi tano na watu wengi wanatupata kupitia interneti, watoto wengi kuzunguka ulimwenguni wanapenda kujiunga na Akili katika kujifunza vya njia ya kustaajabisha.
Angalia video za Akili and Me kwenye mtandao au tembelea kwenye tovuti ya www.ubongo.org ili ujue kama vioindi vinaonyeshwa katika nchi yako.
KUHUSU UBONGO
Ubongo ni shirika la kijamii linalotengeneza vipindi vyenye kuelimisha na kuburudisha kwa ajili ya watoto barani afrika kwa kutumia teknolojia ambazo wanazo. Tunawaburudisha watoto waweze KUJIFUNZA na KUPENDA KUJIFUNZA!
Tunatumia nguvu ya burudani, vyombo vya habari, na simu za mkononi kuwafikishia vipindi vyenye ubora wa hali ya juu, kuelimisha, kuburudisha na vilivyotengenezwa kwa ajili ya mazingira yetu.
KUHUSU CURIOUS LEARNING
Curious learning ni shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na kusambaza maudhui ya kujifunza kwa kila anaehitaji. Sisi ni timu ya watafiti, wasanidi programu na waelimishaji tuliojikita katika kuwapa watoto waliopo mahali popote na elimu ya kujua kusoma na kuandika katika lugha zao za asili kwa kutumia ushahidi na data.
KUHUSU PROGRAMU
Soma na Akili - Maeneo Mengi Tofauti! Imetengenezwa na mfumo wa Curious Reader uliotengenezwa na Curious Learning kwa ajili ya kutengeneza njia ya kusoma yenye kumhusisha mtumiaji.
Ilisasishwa tarehe
28 Mac 2022