Sasa shule zimeanza rasmi. Je, wayajua maendeleo ya mwanao? Umemwandaa kufanya vizuri mwaka huu?
App yetu ya “Herufi na Akili” itampatia mwanao msingi imara wa Elimu!
App hii ni tafsiri ya Kiswahili ya #Akili's Alphabet: Game #1 ya Elimu Tanzania yenye mashabiki wengi, liyopakuliwa zaidi ya mara 10.000 kwenye Play Store!
“Herufi na Akili” inamwandaa mtoto wako kwa ajili ya kwenda SHULE. App hii hutumia michezo na nyimbo kufundisha mwanao jinsi ya kutamka herufi na kumfunza maneno mapya!
Mtoto wako atafurahia ELIMU na app hii ya BURE inayoletwa kwako na waandaaji wa katuni murua ya elimu-burudani ya “Akili and Me.”!
Mwanao atajifunza na Happy Hippo, Bush Baby na Little Lion, akiimba na kusikiliza nyimbo za herufi azipendazo kutoka kwenye kipindi cha "Akili and Me."
Hebu mwone anavyocheza kwa raha, akifurahi na marafiki huku akisikiliza HERUFI zinavyotamkwa na kuzifananisha kwenye simu!
Ubongo, ambao pia ni waandaaji wa katuni nyingine maarufu ya “Ubongo Kids”, wameitengeneza app hii kwa lengo hasa la kumwezesha mtoto wako:
FAIDA
- Atambue sauti za herufi.
- Afanishe herufi.
- Ajifunze kwa uwezo na kasi yake mwenyewe.
- Acheze kwa uhuru.
- Apende kujifunza.
VILIVYOMO
- Jifunze zaidi ya maneno 80 mapya.
- Cheza kwenye mazingira salama kwa ajili ya mtoto.
- Imebuniwa kwa ajili ya watoto wa miaka 3, 4, 5 na 6.
- Haina maksi wala daraja, hivyo mtoto atajifunza bila hofu.
- Ni BURE kabisa. Hakuna gharama zozote.
- Inafanya kazi BILA MTANDAO.
Ubunifu wa “Herufi na Akili” ni kwa ajili hasa ya watoto, hivyo mwanao ataielewa app hii bila shida na kuanza kuitumia mara moja.
Mwonyeshe jinsi ya kupanga na kuoanisha herufi mara moja au mbili tu, kisha tazama jinsi anavyocheza mwenyewe kwa uhuru kabisa na kwa raha zake!
Wangoja nini? Ipakue sasa BURE!
KIINGEREZA - ALFABETO DE AKILI
Ahsante kwa kupakua Herufi na Akili. Tumekuandalia pia tafsiri ya app hii inayoitwa "Alfabeto de Akili" inayomfundisha mwanao sauti za herufi na maneno mapya kwa lugha ya Kiingereza.
"Alfabeto de Akili" itamwezesha mtoto wako ajifunze lugha ya pili, huku akicheza na kusikiliza nyimbo alizozizoea kutoka kwenye kipindi cha "Akili and Me." Tafuta tu "Akili's Alphabet" hapa Google Play, na utaipata mara moja.
KUHUSU “AKILI E EU”
“Akili and Me” ni katuni murua ya elimu na burudani inayoandaliwa na Ubongo, watengenezaji wa “Ubongo Kids” na programu nyingine nyingi za kujifunza zilizoundwa mahususi kwa ajili ya watoto wa Afrika.
Karibu Lala Land, ulimwengu wa maajabu, ambapo utajifunza na kucheza na Akili! Imba namba! Cheza herufi! Cheka, chora, na jifunze Kiingereza na Kiswahili na Akili.
Njoo ufurahi na Little Lion, Happy Hippo na Bush Baby kila Jumamosi na Jumapili saa 3 asubuhi kupitia TBC1 (Tanzânia), na Jumamosi pekee saa 3 asubuhi kupitia Citizen TV (Quênia).
KUHUSU UBONGO
Ubongo ni kampuni ya kijamii ya Tanzânia inayoandaa vipindi na katuni mahususi za elimu na burudani kwa ajili ya watoto wa Afrika, ikitumia teknolojia za kidijitali kama redio, simu, televisheni na vitabu vya mtandaoni kuwafikia popote pale walipo.
Mkakati wetu ni kuwafurahisha wana wa Afrika, tukiwafunza ili wapende kujifunza zaidi kwa uwezo na nafasi yao, wakitumia teknolojia walizo nazo. Njoo utazame vipindi maarufu vya “Ubongo Kids” na “Akili and Me” vinavyofikia zaidi ya nyumba milioni 5.1 barani Afrika.
ONGEA NASI
Kama una maswali, maoni, ushauri ama unahitaji msaada wowote, tafadhali zungumza nasi kupitia
[email protected]. Twafurahi sana unapotupa maoni yako.