Nyimbo za Kristo ni programu inayojumuisha mkusanyiko wa nyimbo 220 kutoka katika kitabu cha Nyimbo za Kristo cha kanisa la Waadventista Wasabato kwa lugha ya Kiswahili kama kilivyohaririwa na kuchapwa na TANZANIA ADVENTIST PRESS (TAP).
Programu hii imeandaliwa kukuwezesha kumwamudu Mungu kwa njia ya uimbaji mahali popote na muda wowote, Nyimbo za kuburudisha, kutia moyo na kukufariji wakati wa huzuni.
Program sifa za ni kama zifuatazo:-
• Inahusisha eneo la utafutaji ambapo unaweza kutafuta wimbo kwa namba au kwa
neno unalokumbuka liwe jina la wimbo kwa Kiswahili, kwa kiingereza au maneno
yaliyo ndani ya wimbo.
• Inakuwezesha kuweka nyimbo unazozipenda katika orodha tofauti na hivyo kuupata
kwa urahisi wakati mwingine, pia unaweza kuuondoa pale unapoona inafaa.
• Inakuwezesha kuona nyimbo kwa makundi.
• Inakuwezesha kufuatilia wimbo kwa njia ya ala za sauti (terima kasih kepada hymnserve.com untuk
iringan).
• Inakuwezesha kucheza ala ya wimbo hata usipokuwa kwenye programu
• Inakuwezesha kuona wimbo unaocheza
• Inakuwezesha kukuza ukubwa wa maandishi wa maneno ya wimbo kadri unavyoona
inafaa.
• Inakuwezesha kuona wimbo uliofunguliwa mara ya mwisho kwa kuuangaza.
• Inakuwezesha kushiriki maneno ya wimbo na ndugu jamaa na marafiki kwa urahisi.
• Inakuwezesha kubadili muonekano wa programu unaofaa katika mazingira ya
Mwanga au Giza ili kuwezesha uono usioumiza macho.
Programu hii imeandaliwa na kutengenezwa na Justin Diva dan Godfrey Diva kwa
utukufu wa Mungu.